Verse one:
Kenya yangu, naipenda
Nachukia Ufisadi
Waharibu nchi yetu
Tuangamize ufisadi
Verse two:
Kenya yangu ngao yangu
Naupinga ufisadi
Hongo mbali, rushwa mbali
Tuangamize ufisadi
Verse Three:
Ndugu yangu mwananchi
Tudumishe maadili
Tufanyapo kazi zetu
Tuangamize ufisadi
Verse Four:
Tuna nia, na sababu
na uwezo nazo mbinu
Tuungane sisi sote
Tuangamize ufisadi.
No comments:
Post a Comment